Submit your work, meet writers and drop the ads. Become a member
ISSAI MASHINGO Jun 2014
Taifa haliwezi kuwa na maendeleo ikosekanapo hekima,
Nchi haiwezi kuwa na chakula pasipo wakulima,
Jamii haiwezi pata maendeleo pasipo kujituma,
Siasa yetu leo ni ya kuwasha na kuzima,
Maneno yasemwayo hayaingii akilini mwa mtu mzima,
Madaraka wanajipatia na vyeo kwa lazima,
Hawajali ya jana wala leo wanajali shibe yao,
Wanalimbikiza mali kwa miradi ya wanao,
Wanaikandamiza haki kwa kutumia elimu yao,
Demokrasia imekuwa kinga yao dhidi ya ufisadi wao,
Siasa imekuwa nyimbo tena zile za mwambao,
Wakisemana kwa mafumbo wanajuana wao,
Wanakaa majukwaani na makubwa yao matumbo,
Mzee alisema fumbo mfumbie mjinga,
Busara na hekima ni kumsikiliza anaye kupinga,
Maana hoja zake zawezekana zikawa za kujenga,
Utajuaje siri ya adui yako bila kumpenda,
Kamwe huwezi kushinda mechi kwa kujua kupiga chenga,
Kamwe huwezi kuwa na nguvu kwa kujitenga,
Naomba tukazane nchi yetu kuijenga,
Tukipamba na maadui maradhi umasikini na ujinga,
Sio kuyasifia mema ili madhaifu kuyapamba,
Ila ukweli kuusema bali tukitumia hekima,
Ikosekanapo kamba huwezi teka maji yakisima,
Ikosekanapo nanga huzamisha meli nzima,
Kuwa na vingi si kuishi kwa kujinyima,
Unapojenga msingi katu huwezi kurudi nyuma,
Mkulima mzuri hutegemea mbivu kuzichuma,
Yule aliye mvivu kamwe hawezi kujituma,
Daima yeye aliye msikivu hujifunza na kuelewa,
Ila Yule aliye mvivu hutegemea ngekewa,
Wanasiasa hulalamika kana kwaamba wanaonewa,
Ukweli ni kwamba wanatumia vibaya uhuru waliopewa,
Daima taifa haliwezi endelea ikosekanapo hekima.
© issai
written in my native language or i should say  my mother tongue the language used is Swahili which is my national language am a Tanzanian for those who don't know where that is found its found its in East Africa if there is an option of translating this please do its a good poem and its my first since i have started writing poetry i have never used Swahili this is my first poem in Swahili.........!!!!!
PETTY POET Sep 2020
NI SAHII*
Nimekuwa silent for a while waka-confuse kuhang boots na a short break,huwezi nipata bar no wonder bars zangu ziko so-bar,black supremacy... Niko na connection na maraga ndio maana akanipea hii ko-r-ti,ni  poet petty siku hizi na-weigh content si  value ya suti,apart from kutema visiriaz,nacheza guitar na at times isukutti,kaa ni kisima,si  unajua obvious hii_ siikuti,

Daily na hood niite mya-hoodie,ni  due to public demand so sikuwa na budi,nilipretend kunguru ndio nipate hizo white collar jobs,na nikasema sitadiss king rabbit ndio unispot kaka,aty petty ameomoka?,si aitane basi sherehe ya kukata na shoka,kaa ni breko naamkia konyangi,na hii  dry spell uko sure hunyongangi?.

Hii class kila mtu  huchoma tuko high class,heri  uko mnakula vako,huku kumekauka kuliko kichwa ya babu owino,dawa ya wivu nakuandikia eno,situmii smartphone natumia phone smart,only call sina  time ya kuchat,ambia smart joker jokes zake huwa joked smart,

Walisema sikio la kufa halisikii dawa,acha nijaribu tena  MARA MOJA, thanks to corona for the first time mluhya anaoga mkono na si  ugali anakula,na petty unatema hata  mtu  haezi sema,ni  venye alikuwa na vinyasa mbili so nikamwomba sho-r-t
moja,na petty pieces zako huniacha in pieces,hizo ndio comments nareply,juz for teases,

Na kama corona shida zangu huwezi zicough out kwa public,natumia mouth piece ya scimo na Leo hatubongi za mitaro na toothpicks,na kuna chizi flani  ananukia colon na hii corona huwezi sema kwa mama mboga iko loan,na kama ni  lyrics nauza hii itabidi umechomoa mita,na before niachilie mic,kumbuka sonko alisema social distance ni  ya one metre,sihang suspenders kwa shoulders, nikiwa hustle nahang guitar,hio  time short nimespend apa  nilikuwa na blessings za mama no wonder sijastammer,kama nimekubamba scratch kwa tenje uniseti stage ndio home na sijaplan...kuhama.
-P€TT¥PO€T✍️
©️2020.
PETTY POET Jul 2020
Before uende tizi,usikule ndizi,that could make you feel uneasy,nowadays injili naspread bila bibles,the only player kwa hii game anacheza na bi-*****,hii si  kujichocha ni  vile skills nimeobtain kwa makocha,luku safi na maganji kwa toja,na hi I dunia ni ya sir God so kaa unategea downfall yangu my friend utangoja.

Art inatoka kwa heart,PETTY POET is about to change ile narrative imekuwepo,my lines are full of flavour kaa ni diss unapokea kichapo,ni  heri uko mnaeza kula vako,huku kumekauka kuliko kichwa ya babu owino,na Jana na Leo mayutt daily ni  kilio,promises hamfulfill kisha kwa mbulu unabrag venye  uko na spirit ya kuokolea,zote mauongo,I wish ningekuwa na kalamu ni-underline na rangi iliyokolea.

Kama ni  uhondo unatafuta songea,si kubrag ni course ya success nilisomea,daily  nikiota nagrow ka mmea,kila mtu  ana-views tofauti huwezi sikia nikikusemea,ukibehave abnormally tunakutreat normally,si  wasapere pekee wanapenda mali ata  mayoh utaskia wakisema no-mali,

Hii time short nimespend apa  nilikuwa na blessings za mama no wonder sijastammer,kama nimekubamba scratch kwa tenje uniseti stage name sijaplan kuhama.
Follow PETTY POET on;
YouTube;PETTY POET
Instagram;POET_PETTY
Twitter;@PETTY POET
Facebook;https://www.facebook.com/105361811084811/posts/157686379185687/?app=fbl
Writco.com;PETTY POET
Mdundo.com;PETTY POET
Whatsapp/tell;0781967348
Tell2;0713434887

— The End —