Submit your work, meet writers and drop the ads. Become a member
Jan 2016
Hapa ndipo umenifikisha
Umalenga na ujopo
Wa kiingereza tulimudu
lakini kiswahili kitamu
**** la mama litamu
Hata liwe la mbwa

Kimombo kilaini majineno
Kama mayai ya johari
Kuangaza mitima halaiki
Namshukuru Rabuka
Kwa talanta ya kuandika

Tukaumba kwa maneno
Waumbaji nikawaunga
Kama yeye Mungu,
Nguvu za maneno kat'tunukia

Uwezo wa karana hii
Kuwateka akilizo
Nyika na mito kuwavusha
Hadi sayari za ndoto zao
Uswahilini narudi mie
Kitamu kwelikweli

Nashukuru Maulana
Kipaji nilipata
Naye ataniauni
Dau langu lifike kilindini
Nitue kileleni

Niangaze kama Zuhura
Hapa ndipo nimefika
Umalenga na ujopo
N'taukumbatia milele
Kwa Kiswahili na kimombo

Mitima zao kusisimua.
Standby for translation...
Written by
andrew juma  universal
(universal)   
2.2k
     SassyJ and Jemoh
Please log in to view and add comments on poems