Submit your work, meet writers and drop the ads. Become a member
andrew juma Jan 2016
Hapa ndipo umenifikisha
Umalenga na ujopo
Wa kiingereza tulimudu
lakini kiswahili kitamu
**** la mama litamu
Hata liwe la mbwa

Kimombo kilaini majineno
Kama mayai ya johari
Kuangaza mitima halaiki
Namshukuru Rabuka
Kwa talanta ya kuandika

Tukaumba kwa maneno
Waumbaji nikawaunga
Kama yeye Mungu,
Nguvu za maneno kat'tunukia

Uwezo wa karana hii
Kuwateka akilizo
Nyika na mito kuwavusha
Hadi sayari za ndoto zao
Uswahilini narudi mie
Kitamu kwelikweli

Nashukuru Maulana
Kipaji nilipata
Naye ataniauni
Dau langu lifike kilindini
Nitue kileleni

Niangaze kama Zuhura
Hapa ndipo nimefika
Umalenga na ujopo
N'taukumbatia milele
Kwa Kiswahili na kimombo

Mitima zao kusisimua.
Standby for translation...
rahim Mar 10
Leo mapema nikupe stori wa ubavu upate kucheka,
Na  jioni sana upike mtori mashavu yapate kumeta,
koroboi mama tuvike nyavu na kagiza tupate kwa mkeka,
Hoi na uchovu mbwa koko nawai nyumbani nipate  kubweka.
1
👉

— The End —