Hello Poetry
Submit your work and get some sparkles! Create free account
Chini ya mnazi bandarini Kumbukumbu ndizo zilizobakia tu Kunizinguka akilini Huba lako kulikosa Yaumiza moyoni Upepo kutoka baharini Tulipoketi ukininong'onezea Sikioni kwamba ni mimi tu Kwamba utanipenda Tukichora zetu mchangani Aaah, nyakati za raha hizo! Ukaniliwaza mtima Tukapanga mipango ya milele Nabakia kutafuna utamu Wa kumbukumbu tu Chini ya mnazi bandarini Nikilemewa maradhi ya moyo Filamu ya huba letu akilini Tukicheza ufukoni Penzi ndio madini ninayokosa mwilini Kama kosa ni langu najuta Usinkwepe rejea nakwita Nitakuenzi nikutunze almasi Tulitwae tunda la penzi nawe Tulichovye buyu la asali Wengine waone kijicho Tupendane tena Chini ya mnazi bandarini
0
Jan 10, 2016
Jan 10, 2016 at 3:07 AM UTC
Rejea Mpenzi

Come back sweet love! Translation's up next...
Written by
Jan 10, 2016
Jan 10, 2016 at 3:07 AM UTC
Request permission to use this poem