"sio" poems
Taifa haliwezi kuwa na maendeleo ikosekanapo hekima,
Nchi haiwezi kuwa na chakula pasipo wakulima,
Jamii haiwezi pata maendeleo pasipo kujituma,
Siasa yetu leo ni ya kuwasha na kuzima,
Maneno yasemwayo hayaingii akilini mwa mtu mzima,
Madaraka wanajipatia na vyeo kwa lazima,
Hawajali ya jana wala leo wanajali shibe yao,
Wanalimbikiza mali kwa miradi ya wanao,
Wanaikandamiza haki kwa kutumia elimu yao,
Demokrasia imekuwa kinga yao dhidi ya ufisadi wao,
Siasa imekuwa nyimbo tena zile za mwambao,
Wakisemana kwa mafumbo wanajuana wao,
Wanakaa majukwaani na makubwa yao matumbo,
Mzee alisema fumbo mfumbie mjinga,
Busara na hekima ni kumsikiliza anaye kupinga,
Maana hoja zake zawezekana zikawa za kujenga,
Utajuaje siri ya adui yako bila kumpenda,
Kamwe huwezi kushinda mechi kwa kujua kupiga chenga,
Kamwe huwezi kuwa na nguvu kwa kujitenga,
Naomba tukazane nchi yetu kuijenga,
Tukipamba na maadui maradhi umasikini na ujinga,
Sio kuyasifia mema ili madhaifu kuyapamba,
Ila ukweli kuusema bali tukitumia hekima,
Ikosekanapo kamba huwezi teka maji yakisima,
Ikosekanapo nanga huzamisha meli nzima,
Kuwa na vingi si kuishi kwa kujinyima,
Unapojenga msingi katu huwezi kurudi nyuma,
Mkulima mzuri hutegemea mbivu kuzichuma,
Yule aliye mvivu kamwe hawezi kujituma,
Daima yeye aliye msikivu hujifunza na kuelewa,
Ila Yule aliye mvivu hutegemea ngekewa,
Wanasiasa hulalamika kana kwaamba wanaonewa,
Ukweli ni kwamba wanatumia vibaya uhuru waliopewa,
Daima taifa haliwezi endelea ikosekanapo hekima.
© issai
Jun 26, 2014
Jun 26, 2014 at 6:04 AM UTC
Mtu mweusi mweusi, katika mwezi mkali wa moto,
ameketi katika kivuli cha mti wa Baobab.
Majani yaliyomo mara moja
walikuwa kavu na ukame,
waathirika wa upepo wa mabadiliko.
"Wazee, wananiita zamani." Alidhani,
"Majira ya joto ya sabini yanigeuka kijivu,
lakini mti huu wa Baobab ulikua mrefu na wenye nguvu
Wakati majeshi ya Kirumi yalipitia njia hii. "
Mzee huyo alitafuta matunda ya baobab
na akaingia kwenye hali kama hali.
Alikuwa katika hali ya akili;
Sio usingizi, sio macho kabisa.
Aliposikia sauti: "Nina kiu." Ilisema,
Ingawa alikuwa na uhakika alikuwa peke yake.
Ilionekana si sauti ya binadamu:
monotone kavu ya ubongo.
"Kwa vizazi, wanaume kama wewe
Walitaka makazi yangu kutoka kwenye jua,
Lakini sasa imekamilika; nchi imeharibika
Na mimi nina kufa, mdogo. "
Mtu mzee alilia kusikia maneno haya
Kwa maana miti hizi zinapokufa, kama lazima,
Wao huanguka juu ya ardhi yenye ubongo
Hivyo haraka kurudi kwenye Vumbi.
"Dunia imebadilika kwa wewe na mimi,
Upepo ni kavu chini ya jua.
Ninasamehe ulimwengu wa wanadamu
Kwa maana hawajui waliyofanya. "
Mtu mzee aliamka na mwanzo
na akainua na miwa yake.
Alilia kwa kufikiri mti huu utafa
lakini machozi hawezi kuchukua nafasi ya mvua.
Jun 21, 2018
Jun 21, 2018 at 7:50 AM UTC
Ungali futa subira tu
Hali yangu mbaya imefanya umenikimbia
Sina, hope, nilikuambia?
mapenzi yakweli nilikupa sio kutania
Marafiki wanakuulizia niwaambie nini ?
Nimekuzoea siungelitulia.
Alafu moyo unaujinga bado unakuhitaji
Aug 30, 2018
Aug 30, 2018 at 5:48 PM UTC