"mungu" poems
Hapa ndipo umenifikisha
Umalenga na ujopo
Wa kiingereza tulimudu
lakini kiswahili kitamu
**** la mama litamu
Hata liwe la mbwa
Kimombo kilaini majineno
Kama mayai ya johari
Kuangaza mitima halaiki
Namshukuru Rabuka
Kwa talanta ya kuandika
Tukaumba kwa maneno
Waumbaji nikawaunga
Kama yeye Mungu,
Nguvu za maneno kat'tunukia
Uwezo wa karana hii
Kuwateka akilizo
Nyika na mito kuwavusha
Hadi sayari za ndoto zao
Uswahilini narudi mie
Kitamu kwelikweli
Nashukuru Maulana
Kipaji nilipata
Naye ataniauni
Dau langu lifike kilindini
Nitue kileleni
Niangaze kama Zuhura
Hapa ndipo nimefika
Umalenga na ujopo
N'taukumbatia milele
Kwa Kiswahili na kimombo
Mitima zao kusisimua.
Jan 6, 2016
Jan 6, 2016 at 8:03 AM UTC
NAKUSHUKURU
Baba nakushukuru kwa kunipa uhai hata sasa,
Nashukuru kwa kunisamehe na kunitakasa,
Nashukuru kwa kuwa ulikufa kwa ajili yangu,
Nashukuru kwani ulinibariki toka tumboni mwa mama yangu,
Nashukuru unanipenda hata na mapungufu yangu,
Nashukuru kwa kuwa unanilinda kutoka na kuingia kwangu,
Lihimidiwe jina lako YEHOVA hakuna kama wewe,
Mungu kwa kuwa hakuna kinachoweza kulinganishwa na upendo wako,
Hakuna kinachoweza kulinganishwa na wema wako,
Je ni mwanadamu gani awezaye kufa kwa ajili ya asimjua?
Ni nani awezaye kukubali kuteseka kwa niaba ya yule amchukiaye?
Ni nani awezaye kuuweka chini uhai wake kwa ajili ya adui yake?
Jun 26, 2014
Jun 26, 2014 at 6:07 AM UTC